Maafisa wa ardhi wanaoshiriki katika kutowa stakabadhi ya ardhi ya unyakuzi kushtakiwa
mohamed kombo
July 21, 2026
NEWS
Maafisa wa ardhi ambao wanahusika katika zoezi la unyakuzi wa ardhi nchini watachukuliwa hatuwa za kisheria .
Akizungumza katika kaunti ya Kisumu afisa mkuu mtendaji wa tume ya kupambana na ufisadi nchini (EACC ) Abdi Ahmed Mohamud amesema kando na kurejesha ardhi za umma ambayo yamenyakuliwa wataweza kuchukulia hatuwa maafisa wa idara ya ardhi ambao walihusika katika zoezi la kutowa stakabadhi ya ardhi iliyonyakuliwa .
Kulingana na Mahmoud ardhi ya idara ya magereza iliyoko katika kaunti ya Kisumu eneo la Winam Estate ilkuwa ya ekari 16 imeweza kunyakuliwa na wakenya ambao wanadai wao ndio wamiliki wa ardhi hiyo na sasa imesalia sehemu ndogo .
Amewataka waliyo na hati miliki ya sehemu ya ardhi hiyo ambayo imesalia wazi kuweza kurejesha kwa EACC akisema wata akikisha ardhi za umma zilizo nyakuliwa kuweza kuregeshwa kwa serekali .
EACC inalenga kuregesha ardhi hiyo ambayo ni ya ekari 7.6 ambayo iko katika makazi ya winam akisema ardhi hiyo ambayo ilinyakuliwa 1980 ni ya thamani ya shillingi milloni 790.
Back to News