Wakazi wa Kisumu watakiwa kuwa makini wanaponunuwa shamba
mohamed kombo
July 21, 2026
NEWS
Wakazi wa Kisumu wameonywa dhidi ya ununuzi wa Mashamba kabla ya kufanya utafiti na kujuwa wamilki halisi wa amshamba hayo .
Ni wito ambayo umetolewa na kaunti kamissoner wa Kisumu Ramadhan Mwabudzo.
Mwabudzo amehimiza wakazi kuzuru afisi ya ardhi ,kuchunguza majirani ambao wanaishi kando ya ardhi pamoja na ramani ya ardhi hizo na mipango ya ardhi na mji kabla ya kununuwa ardhi yoyote .
Amewataka wakazi pia kufuata mchakato wa kisheria wanapotafuta hati miliki akionya kuwa yoyote atakaye nyakuwa ardhi ya umma atashtakiwa.
Kulingana na Mwabudzo unyakuzi wa ardhi katika kaunti ya Kisumu imekithiri ikwiemo ardhi ya wizara nyumba ,ardhi ya mamlaka ya reli ,ardhi ya idara ya mahakama ,Taifa Park na ardhi ya uwanja wa ndege miongoni mwa ardhi zengine kati kati mwa jiji la Kisumu.
Amesema haya katika mukutano ambayo pia uliudhuriwa na mwenyekiti wa muungano wa waislamu Kisumu Sheikh Musa Ismali .
Back to News