Msikiti wa Jamia Isebania kuwa miongoni mwa msikiti mkubwa eneo la Nyanza
Mohamed Kombo
July 12, 2026
NEWS
Mji wa mpaka wa Isebania kaunti ya Migori ni moja ya eneo ilyo na msikiti mkubwa katika eneo la Nyanza baada ya kufunguliwa kwa msikiti mpya eneo hilo.
Msikiti huo uliyo na nafasi ya kubeba idadi ya waumini 2000 unatarajiwa kwa kitovu cha ibaada cha Ibaada katika eneo la Isabania ambayo iko katika mpaka wa Tanzania na kusadia katika kuelimisha jamii .
Kulingana na mbunge wa Suna mashariki Junet Mohammed ambaye alizungumza wakati wa ufunguzi wa msikiti huo aliweza kuhimzia waumini wa dini ya kislamu kutumia msikiti huo kudumisha amani ,uvumilivu na heshima miongoni mwa dini zengine .
Junet ameahidi msikiti mwengine mkubwa kuweza kujengwa katika mji wa Migori kama njia ya kueneza dawaah katika eneo la Nyanza .
Gavana wa wajir Ahmed Abdullahi kwa upande wake amehmiza wakazi wa eneo la Isebania kuwa mabalozi wa dini ya Kislamu ili kuweza kuvutia wasiyo kuwa wasilamu katika dini.
Akizungumza katika hafla hiyo gavana wa Migori Ochilo Ayako aliweza kutowa wito kwa waislamu katika kaunti hiyo kuweza kutuma maombi ya nafasi ya ajira ambayo imetengazwa katika kaunti hiyo
Back to News